- 4,813 viewsDuration: 3:31Viongozi wa Kenya Kwanza kwa mara nyingine wameendelea kumfokea Rais mstaafu Uhuru Kenyatta wakisema juhudi zake za kutumia wanasiasa wa upinzani kutwaa uongozi wa taifa hazitafaulu. Viongozi hao waliokongamana katika hafla tofauti za kupiga jeki makundi mbalimbali kule Busia, Kericho, Kuresoi na Kaunti ya Uasin Gishu wanasema serikali iko imara na imeweka mipango maalum ya kutwaa uongozi wa taifa kwa mara nyingine katika uchaguzi mkuu ujao.