- 919 viewsDuration: 3:57Viongozi wa kidini jioni hii wametoa wito wa amani siku mbili kabla ya kumbukumbu za waathiriwa wa maandamano dhidi ya serikali yaliyoshuhudiwa nchini Juni 25 miaka miwili iliyopita. Viongozi hao sasa wakiitaka serikali pamoja na wenzao wa upinzani kuweka kando tofauti zao na badala yake kufanya mazungumzo ambayo yatazuia machafuko yoyote ya taifa. Aidha wamewarai walinda usalama kutotumia nguvu endapo maandamano haya yatafanyika.