- 349 viewsDuration: 1:54Baadhi ya viongozi kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya, wakiongozwa na Kenneth Lusaka, wamewahimiza wakazi kujisajili kama wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Viongozi hao pia wameeleza kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa William Ruto, wakisema eneo hilo bado lina idadi kubwa ya wananchi ambao hawajajiandikisha kupiga kura na kuwataka kuhakikisha majina yao yanaingizwa kwenye daftari la wapiga kura ili kuongeza ushiriki wa eneo hilo katika uchaguzi na kuimarisha uwakilishi wake.