- 1,448 viewsDuration: 1:53Viongozi wa serikali jumuishi wameendeleza kampeni za kumpigia debe rais William Ruto, wakisema ameimarisha hadhi ya maisha ya mkenya wa kawaida. Mrengo wa Kenya kwanza ukiongozwa na naibu rais Kithure Kindiki, ulisema kuwa sekta ya kilimo imeimarika pakubwa katika miaka minne iliyopita ikiwemo ufufuaji wa viwanda vya sukari pamoja na kupungua kwa bei ya mbolea na mbegu ili kuhakikisha lishe ya kutosha. viongozi wa ODM nao wamewakashifu viongozi wa upinzani wakisema wanaendeleza semi za chuki. Viongozi hao walihudhiria hafla mbali mbali kaunti za Migori, Busia, Vihiga, Meru na Bungoma.