Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa serikali washambulia upinzani kwa kulalamikia IEBC

  • | Citizen TV
    1,536 views
    Duration: 2:58
    Viongozi wanaounga mkono serikali wamewataka wenzao wa upinzani kuwacha lalama za mara kwa mara kuhusu utendakazi wa tume ya uchaguzi nchini IEBC, na badala yake kujiandaa kwa makabiliano makali debeni. Wakizungumza katika kaunti za Transnzoia na Narok, Viongozi hao pia wamedai wapinzani wa serikali wanakerwa na tume hio kwa kunyimwa zabuni za kuisambazia bidhaa tofauti, kabla ya uchaguzi mkuu.