- 834 viewsDuration: 2:15Viongozi wanaounga mkono serikali wameendelea kuwakashifu wapinzani kutokana na madai yao kuhusu utendakazi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC. Viongozi hao wanasema upinzani unalenga kuondoa imani ya wananchi kwa tume hiyo kabla ya uchaguzi. Aidha, wametetea rekodi ya maendeleo ya Rais William Ruto, wakisema wananchi wanapaswa kuzingatia mafanikio ya serikali katika kipindi chake cha kwanza na kumpa kura katika uchaguzi ujao.