Viongozi wa upinzani wameitaka serikali kuhakikisha haki inatendeka kwa waathiriwa wa maandamano huku wakisifia kile walichodai kuwa mafanikio ya maandamano ya amani ya Alhamisi iliyopita.
Viongozi hao, wakiwemo Kalonzo Musyoka wa Wiper na Eugene Wamalwa wa DAP-K, wamesema fidia ya pesa pekee haitoshi na kwamba waliohusika na ukiukaji wowote wa sheria wanapaswa kuwajibishwa kisheria.
Aidha, wameikosoa kauli ya Rais William Ruto dhidi ya kampuni ya habari ya Standard.
Wanasiasa hao walizungumza katika kaunti ya Kajiado walikohudhuria ibada ya Jumapil