Skip to main content
Skip to main content

Viongozi waonya kuhusu utayari wa uchaguzi mkuu

  • | Citizen TV
    1,171 views
    Duration: 2:38
    Katika taarifa nyingine, viongozi wa kidini pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu sasa wanasema wana wasiwasi kuhusu utayari wa Tume ya Uchaguzi katika kuandaa uchaguzi mkuu ujao. Kwenye kikao cha wadau mbalimbali wa uchaguzi, viongozi hao pia wameelezea dukuduku kuhusu joto la kisiasa linaloshuhudiwa nchini, hasa kile wanachokitaja kuwa utepetevu wa idara za serikali katika kukabiliana na wahuni na wanasiasa wachochezi.