Skip to main content
Skip to main content

Visa vya Ebola Kenya vyafikia 7, KMPDU yaikosoa Wizara ya Afya

  • | Citizen TV
    5,132 views
    Duration: 3:07
    Idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Kenya imefikia 7. Hii ni baada ya Wizara ya Afya kuthibitisha visa vingine 4 vya Ebola. Miongoni mwao ni wahudumu watatu wa afya waliomhudumia mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini, ambaye aliaga dunia tarehe 5 mwezi wa Oktoba mwaka huu. Wizara ya Afya imesema wanne hao wamekuwa katika vituo vya kuwatenga washukiwa wa ugonjwa wa Ebola tangu tarehe 9 mwezi huu. Na kama anavyoarifu sasa Serfine Achieng Ouma, Muungano wa Madaktari Nchini (KMPDU) umeishutumu Wizara ya Afya kwa kukosa kuwahusisha madaktari kwenye mipango ya kitaifa ya kukabiliana na Ebola.