- 1,002 viewsDuration: 1:17Kampuni ya Viutravel imeshirikiana na Ubalozi wa Barbados nchini kuitangaza nchi hiyo kama eneo bora kwa Wakenya kutalii. Ushirikiano huo umetiwa saini na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati katika Mamlaka ya Utalii ya Barbados, Kyle Gittens, pamoja na Kui Muriithi wa Viutravel. Viutravel pia imezindua kampeni ya safari itakayofanyika kati ya tarehe 3 na 10 Novemba mwaka huu. Wakenya wanaosafiri kwenda Barbados hawahitaji visa ya kuingia nchini humo, hatua inayotoa fursa kwa wanaotaka kutalii eneo hilo.