- 14,730 viewsDuration: 3:29Waandamanaji 355 wamekamatwa leo kufuatia maandamano ya amani yaliyoandaliwa kuadhimisha kumbukumbu ya Juni 25 kwa ajili ya kuwakumbuka vijana waliouawa miaka miwili iliyopita. Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amesema serikali imeridhishwa na namna maandamano ya leo yalivyoendeshwa. Hata hivyo, mvutano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji ulishuhudiwa katikati ya jiji la Nairobi huku shughuli zikitatizika kwa muda.