Skip to main content
Skip to main content

Waandamanaji sita waliotoweka wapatikana

  • | Citizen TV
    7,873 views
    Duration: 4:03
    Waandamanaji sita waliotoweka wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu za Juni 25 wamepatikana. Watatu walitelekezwa katika barabara ya Lang’ata huku wengine watatu wakipatikana katika msitu wa Ngong. Wote walidai kupigwa vibaya na kwa sasa wanapokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi Women’s. Waathiriwa wanasema walikamatwa kwa nguvu na kupakiwa kwenye lori la polisi, wakazungushwa katika maeneo mbalimbali kabla ya kukabidhiwa kwa wanaume waliovaa barakoa. Kisha walilazimishwa kuingia kwenye magari ya Subaru na kuendelea kupigwa katika vyumba vya siri kabla ya kuachiliwa baadaye.