- 196 viewsDuration: 1:52Uharibifu wa makazi ya wanyama pori umetajwa kama chanzo kikubwa cha migogoro baina ya wanyama na binadamu nchini. Katibu wa uhifadhi katika idara ya wanyama pori Dkt. John Kipkorir Chumo amesema kuongezaka kwa idadi ya watu kumechangia uharibifu wa mazingira na kusababisha wanyama kuingia maeneo ya makazi ya binadamu hali inayohatarisha maisha yao. Akizungumza mjini Hola wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi milioni 172 kwa familia 225 zilizopoteza wapendwa wao kutokana na kushambuliwa na wanyama pori, Chumo amesema idara hiyo inatumia hadi shilingi bilioni moja kila mwaka kama fidia kwa mashambulizi ya wanyama pori.