- 3,848 viewsDuration: 2:31Na huku maafisa wa usalama wakiendelea na uchunguzi kuhusu kilichotokea katika shule ya wasichana ya Utumishi Academy, Gilgil, washikadau wa elimu sasa wanaelekeza kidole cha lawama kwa serikali. Chama cha walimu na taasisi za masomo KUPPET kimesema serikali imeshindwa kutekeleza kikamilifu kanuni zake kuhusu usalama shuleni. Na kama anavyoripoti Brenda Wanga, serikali imekuwa ikichapisha miongozo ya usalama kila mara baada ya kutokea kwa mikasa ya moto shuleni, hatua inayozua maswali kuhusu utekelezaji wake.