Skip to main content
Skip to main content

Wafanyakazi wa Machakos washinikiza kupitishwa kwa bajeti

  • | Citizen TV
    322 views
    Duration: 1:23
    Wafanyakazi wa Kaunti ya Machakos waliandamana leo kulishinikiza Bunge la Kaunti hiyo kuidhinisha bajeti ya mwaka 2026/2027 ya shilingi bilioni 19. Kupitia miungano mbalimbali, wafanyakazi hao waliishutumu serikali ya kaunti kwa vita vya ndani vinavyoathiri utendakazi wao. Baadhi yao wanadai mishahara ya zaidi ya miezi mitatu, huku wakisema kuwa mtafaruku huo umesababisha kutolipwa kwa mshahara wa mwezi Juni. Naibu Spika wa Bunge hilo aliwalaumu baadhi ya wanasiasa aliodai wanaingilia uhuru wa Bunge la Kaunti.