Skip to main content
Skip to main content

Wafanyibiashara kwenye soko la Kongowea wasajiliwa kuwa wapiga kura

  • | Citizen TV
    274 views
    Duration: 1:13
    Siku moja baada ya tume uchaguzi na mipaka kuanzisha zoezi la usajili wa wapiga kura mjini Mombasa, hamasiho hilo limeingia katika mitaa ya Kongwea, lengo kuu likiwa kuwasajili wafanyabiashara pamoja na wakazi wanaofika kununua bidhaa. Katika hamasisho hilo, wakazi hasa vijana, wamehimizwa kutumia fursa hiyo kujisajili kama wapiga kura ili kuwachagua viongozi watakaoafikia malengo yao ya maendeleo. Baadhi ya wafanyabiashara wa kongwea wamesifia hatua hiyo wakisema changamoto ya kazi na utafutaji wa tonge ndio sababu kuu ya kukosa kujisajili. Sasa wanapendekeza tume ya uchaguzi kuingia nyanjani ili kuwasajili wakenya zaidi.