- 571 viewsDuration: 3:58Tangu kuzinduliwa kwa mpango wa wahudumu wa afya ya Jamii, mwaka wa 2023, wahudumu hao wamekuwa kiungo muhimu katika familia na vituo vya afya, kwa kupeleka huduma za msingi za afya karibu na wananchi. Huko Aldai katikaKaunti ya Nandi, umuhimu ya mpango huo unaonekana katika jamii, huku wahudumunwa afya ya jamii wakiwasaidia kina mama wajawazito kupata huduma za kliniki na uzazi kwa wakati, pamoja na kuwawezesha wakazi kujiandikisha katika Mamlaka ya Afya ya Jamii, SHA.