- 952 viewsDuration: 2:20Kama njia ya kushabikia kupunguka kwa visa vya uhalifu katika eneo la Kiamutugu kaunti Kirinyaga, wakaazi wamejumuika pamoja kuwaaandalia karamu maafisa wa polisi wanaohudumu eneo hilo. Wakati wa sherehe hiyo iliyoandaliwa katika kituo cha polisi cha eneo hilo, wakaazi wametakiwa kujitokeza kama mashahidi baada ya wahalifu kukamatwa, ili kuhakikisha wameondolewa katika ya jamii, na usalama wao kuimarishwa hata zaidi.