- 1,073 viewsDuration: 3:11Zaidi ya miaka 60 tangu Kenya kujinyakulia uhuru hatimaye wakazi 2,500 wa vijiji vya Barageiwet, Kesainet na Sigowet katika eneo bunge la Soin/Sigowet, Kaunti ya Kericho, wanasherehekea uzinduzi wa mradi wa umeme katika eneo hilo. Kwa baadhi ya wakazi ni mara ya kwanza wanapata umeme nyumbani mwao huku Serikali ikisema mradi huo ni sehemu ya mpango wa kupeleka umeme kwa maelfu ya familia nchini.