Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Morita walalamikia ukosefu wa usalama

  • | Citizen TV
    2,216 views
    Duration: 2:13
    Wakazi wa eneo la Morita, Kaunti ya Pokot Magharibi, wamelalamikia ukosefu wa usalama, wakidai kuwa wahalifu kutoka maeneo jirani wamekuwa wakivamia eneo hilo na kuwaua raia wasio na hatia. Kisa cha hivi majuzi ni mauaji ya wanawake wawili wajawazito waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka sokoni. Wakazi hao wanadai kuwa zaidi ya watu saba wameuawa katika kipindi cha chini ya siku saba, huku wakilitaka serikali kuimarisha usalama na kukomesha mauaji hayo.