Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Nyamira wahimizwa kujisajili kwa bima ya SHA

  • | Citizen TV
    119 views
    Duration: 1:30
    Idara ya afya katika kaunti ya Nyamira imewataka wakazi wa kaunti hiyo kujisajili katika bima ya SHA, ili kuwawezesha kupata dawa bila malipo wanapotafuta huduma katika hospitali za umma kwenye kaunti hiyo. Waziri wa afya katika kaunti ya Nyamira Donald Mogoi, amesema watakaofika hospitalini bila kadi ya SHA watalazimika kugharamia malipo ya dawa. Dkt. Mogoi amesema idara ya afya katika kaunti hiyo imezindua mfumo mpya wa kununua dawa katika hospitali za kaunti na kwamba kuanzia sasa hakuna mgonjwa atakayetarajiwa kununua dawa kwingine baada ya kupokea matibabu katika hospitali za umma.