- 27,503 viewsDuration: 2:48Idadi kubwa ya wapigakura ilionekana katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou ambako pia makundi ya wakazi yalionekana kuzingira vituo vya kupiga kura katika eneo bunge hilo. Wakazi hawa wakisema hatua yao imesababishwa na kukosa kwao imani na tume ya uchaguzi ya IEBC. Polisi walikuwa na wakati mgumu kutawanya makundi hayo, ambayo yalikagua magari yaliyokuwa yakiingia katika vituo hivyo, mara nyingine kuwalazimisha maafisa wa tume kutembea. Laura Otieno sasa anaarifu kuhusu zoezi la upigaji kura lilivyokuwa Ol Kalou