- 3,065 viewsDuration: 3:27Bajeti ya mwaka wa 2026/27 imepokelewa shingo upande na mamilioni ya Wakenya wanaolalamika kuwa gharama ya maisha inazidi kupanda bila mikakati thabiti ya kuwakinga. Wafanyabiashara wadogo wanasema licha ya ahadi za serikali, mapato yamepungua huku fedha wanazopata zikielekezwa kwa chakula, kodi, karo za shule na matibabu bila ya akiba yoyote.