Serikali ya kaunti ya Kwale kupitia idara ya kilimo na uvuvi imesema inaweka mikakati ya kuinua kilimo cha mwani ambacho kingali chini ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika Mashariki, kwa sasa kaunti hiyo ikizalisha tani 146 pekee kila mwaka.
Akizungumza katika kongamano la wadau na watafiti katika sekta ya uvuvi huko Diani, waziri wa kilimo katika kaunti hiyo Roman Shera, amesema wanaanzisha ukulima wa aina tofauti ya mwani unaotoa mazao mengi zaidi.
Mashirika ya utafiti katika sekta hiyo yakiwemo Kilimo Trust na KMFRI yakisema kina mama na vijana wamekuwa kwenye mstari wa mbele katika kilimo cha zao hilo.