- 231 viewsDuration: 1:45Masomo katika shule za chekechea (ECDE) katika Kaunti ya Nandi huenda yakaathirika kuanzia kesho baada ya walimu kutangaza mgomo kutokana na mazingira duni ya kazi na kutotekelezwa kwa matakwa yao kwa muda mrefu. Wakizungumza mjini Kapsabet, walimu hao wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya juhudi za kutafuta suluhu kupitia mazungumzo kukosa kuzaa matunda.