Skip to main content
Skip to main content

Walimu wa Kajiado chini ya KUPPET watishia kugoma

  • | Citizen TV
    198 views
    Duration: 2:01
    Chama cha Kutetea Masilai ya walimu wa shule za Sekondari na Vyuo vya Kadri KUPPET Tawi la Kajiado kinatishia kuanza mgomo iwapo serikali haitajitokeza na kuwapa sikio kuhusu matakwa yao ikiwemo malalamishi kwenye bima ya afya ya SHA. Wakihutubia wanahabari katika mji wa Isinya Kaunti ya Kajiado Viongozi wa chama hicho wanasema sehemu nyingi ya mashinani ya Kajiado bima hiyo haifanyi kazi, huku pia wakidai inagharamia kiwango kidogo cha fedha ikilinganishwa na Bima ya minet wlaiyotumia awali.