Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi 300 wa Olubi wakabiliwa na uhaba wa madarasa

  • | Citizen TV
    1,128 views
    Duration: 3:46
    Ni ndoto ya kila mzazi kumuona mwanawe akisoma katika mazingira bora na salama. Hata hivyo, kwa zaidi ya wanafunzi 300 wa Shule ya Msingi ya Olubi kaunti ya Kajiado, ndoto hiyo bado iko mbali kutimia kwani shule hiyo ina majengo mawili na madarasa manne pekee. Madarasa haya hayatoshi, huku walimu wakilazimika kusomesha kwa pamoja ndani ya kanisa waliyopewa hifadhi. Nancy Kering alitembelea shule hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo