- 228 viewsDuration: 2:09Wanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika katika Chuo Kikuu cha Nairobi wameanzisha mtandao wa ushirikiano na ushauri kwa lengo la kukabiliana na changamoto za upweke, msongo wa mawazo na vikwazo vingine vinavyowakumba watafiti. Mpango huo unalenga kuimarisha ustawi wa wanafunzi, kukuza ushirikiano wa kitaaluma na kuwasaidia kukamilisha tafiti zao kwa ufanisi.