Skip to main content
Skip to main content

Wanaharakati wakamatwa Nairobi wakitaka Kanja ajiuzulu

  • | Citizen TV
    3,354 views
    Duration: 41s
    Wanaharakati kadhaa wamekamatwa leo hapa Nairobi baada ya kujifunga minyororo kwenye lango la Jumba la Jogoo, wakishinikiza kujiuzulu kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja. Underlay Wanaharakati hao walibeba majeneza meupe na mabango yaliyomtaka Kanja ajiuzulu. Pia walielezea wasiwasi wao kuhusu madai ya utekaji nyara, mauaji ya kiholela na kile walichokitaja kuwa ni kushindwa kwa polisi kuwalinda Wakenya. Kundi hilo pia lilitaka uwajibikaji na kukomeshwa kwa kile walichokitaja kuwa ukatili wa polisi. Wito huo wa kutaka Kanja ajiuzulu unajiri huku kukiwa na ongezeko la visa vya mashambulizi ya wahuni kwenye mikutano ya kisiasa.