- 2,694 viewsDuration: 1:44Zaidi ya wanajeshi 400 wa zamani wa Jeshi la Anga la Kenya waliohudumu wakati wa jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982, wameungana na Kiongozi wa Chama cha Safina Jimmy Wanjigi kudai kulipwa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni tisa. Wanajeshi hao pia wanataka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Katibu wa Ulinzi Patrick Mwariru kwa madai ya kutotii amri ya mahakama iliyoiagiza serikali kuwalipa fidia. Chama cha Safina pia kimeilaumu serikali kwa kulenga wahamiaji wa kigeni, kikisema haijawajibikia ipasavyo Wakenya wanaokandamizwa.