Wasanii na watayarishi wa vipindi vya mitandaoni nchini huenda wakapata nafuu kubwa endapo mswada wa uchumi wa ubunifu kwa vijana wa mwaka 2025 utapitshwa na Bunge. Katibu wa Wizara ya masuala ya vijana na uchumi wa ubunifu, Fikirini Jacobs, amesema mswada huo uliowasilishwakwa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu michezo unalenga kukuza, kudhibiti na kuwezesha sekta hiyo kuingiza mapato zaidi. Aidha anasema unapaswa kuwalinda vijana wenye vipaji dhidi ya watu wanaowatumia vibaya. Fikirini alikuwa akizungumza wakati wa toleo la pili la hafla ya kila mwaka ya Mr & Mrs Samba iliyoandaliwa Kaunti ya Kwale.