Shabiki.com imewazawadi washindi wa wiki ya pili wa kampeni ya Shabikia World Cup Kishabiki.
Mshindi wa kwanza, Edwin Ochieng kutoka Migori, amejishindia shilingi laki mbili na amesema atatumia fedha hizo kufadhili miradi yake mbalimbali pamoja na shughuli za kilimo.
Derrick Anyula kutoka Busia ameshinda shilingi nusu milioni na anasema atazitumia kuendeleza biashara ya kuuza kuku.
Kwa upande wake, mwanafunzi Querren Muyuka kutoka Kakamega amejishindia shilingi laki tatu ambazo anapanga kutumia kulipa karo na kupanua biashara yake ya mitumba.
Mshindi wa nne ni mkulima Kelvin Muriuki kutoka Meru ambaye amesema atatumia shilingi laki mbili alizoshinda kununua mtambo wa kusambaza maji shambani na kuimarisha shughuli za kilimo.
Kampeni ya Shabikia World Cup Kishabiki inaendelea kupitia jukwaa la Shabiki.com na kuwapa mashabiki wa soka nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni tisa katika msimu huu wa michuano ya Kombe la Dunia.