Mfanyabiashara kutoka Kitengela Polycap Lumumba, Ketry Kusa kutoka Thika na Churchill Oketch kutoka Migori ndio washindi wa mwisho wa kampeni ya Shabikia World Cup Kishabiki baada ya kujishindia jumla ya shilingi milioni moja.
Lumumba alishinda shilingi nusu milioni, Ketry akapata shilingi laki tatu kupitia mchezo wa Crash, huku Churchill akijishindia shilingi laki mbili kupitia Shabiki Sportsbook.
Washindi hao wanasema wanakusudia kutumia fedha hizo kuimarisha maisha yao kiuchumi kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali.