- 1,528 viewsDuration: 2:34Watu saba waliokamatwa kwa madai ya kuhusika katika ghasia za Keumbu hawakufunguliwa mashtaka baada ya mwendesha mashtaka wa kesi kutofika mahakamani. Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Mahakama ya Kisii, Caroline Jeruto, aliamrisha washukiwa hao warejeshwe rumande hadi orodha ya mashtaka yao itakapokuwa tayari. Wakati huo huo, maafisa wa ujasusi wanaendelea na uchunguzi kuhusu ghasia hizo zilizosababisha kifo cha mtu mmoja.