- 2,201 viewsDuration: 1:00Washukiwa wanne wa ujambazi wameuawa huku wawili wakitoroka baada ya makabiliano makali na maafisa wa polisi katika mji wa Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, usiku wa kuamkia leo. Polisi wanasema makabiliano hayo yalizuka kwenye barabara ya Eldoret–Kiplombe, ambako washukiwa walidaiwa kuwaibia wakazi. Kamanda wa Polisi Wilberforce Sicharani amesema washukiwa walikuwa wamevalia sare za kijeshi walipokuwa wakitekeleza uhalifu. Polisi wanaamini walikuwa sehemu ya genge ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa Kitale, Kapenguria, Nandi na Marakwet. Wakati huo huo, msako unaendelea kuwatafuta washukiwa wawili waliotoroka.