- 792 viewsDuration: 3:48Zaidi ya miaka mitano baada ya mzozo wa kijamii kuzuka katika kijiji cha Kambi Samaki, eneo bunge la Lagdera kaunti ya Garissa, shule ya msingi ya eneo hilo imesalia kufungwa. Shule hiyo ambayo zamani ilikuwa kitovu cha elimu katika eneo hilo sasa imegeuzwa kuwa makazi ya maafisa wa usalama, hali inayochangia kuongezeka kwa idadi ya watoto wasiohudhuria masomo kaunti ya Garissa. Wakazi sasa wanaiomba serikali kuongeza idadi ya maafisa wa usalama ili shughuli za masomo zirejelewe shuleni humo.