Skip to main content
Skip to main content

Watoto wawili waliochomwa kwa maji moto kanisani Bondo wahamishiwa Kisumu

  • | Citizen TV
    3,223 views
    Duration: 2:23
    Watoto wawili kati ya wanne waliochomwa kwa maji moto katika kanisa la St. Abraham Israel Assemblies of God, eneo la Bondo, Kaunti ya Siaya, wamehamishiwa Kisumu kwa matibabu ya kitaalamu. Haya yanajiri huku mmoja wa watu wanne waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo akiachiliwa kwa dhamana kutokana na umri wake mkubwa. Kama anavyoripoti Laura Otieno, kundi la Israel Assemblies of God limekashifu vikali tukio hilo, likisema halikuidhinisha mhubiri wa kanisa hilo kufanya matambiko ya aina hiyo.