- 300 viewsDuration: 1:55Watoto wawili waliuawa usiku wa Jumapili katika mazingira ya kutatanisha katika kijiji cha Lokapel, eneo la Katilu, Turkana Kusini. Maafisa wa usalama wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwabaini waliohusika, huku wakazi wakitoa wito wa haki kutendeka na hatua za kuimarisha usalama katika eneo hilo.