- 1,289 viewsDuration: 1:07Maafisa wa polisi mjini Kisii wameanzisha uchunguzi kuhusu ghasia zilizoshuhudiwa katika mazishi yaliyofanyika kijijini Endereti, eneo bunge la Bomachoge Borabu, ambapo watu 10 walijeruhiwa baada ya makundi ya wafuasi waliokuwa wamejihami wa Mbunge wa eneo hilo Obadiah Barongo na Gavana wa Kisii Simba Arati kukabiliana. Tukio hilo linajiri siku chache baada ya kisa kingine cha makundi hasimu kukabiliana katika eneo hilo. Wakazi sasa wanahofia kuwa visa hivyo vinahatarisha usalama wakati huu ambapo joto la kisiasa limeendelea kupanda.