- 1,897 viewsDuration: 2:47Idadi ya waliofariki katika mkasa wa mgodi katika eneo la Romus, Kaunti ya West Pokot, imefikia watu 15. Watu hao waliaga dunia baada ya kufukiwa na vifusi vya mgodi wa dhahabu ulioporomoka katika eneo hilo. Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya Red Cross Society limethibitisha kuwa watu 12 wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kapenguria. Haya yanajiri huku Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen akiwaonya wanaoendesha shughuli za migodi bila kufuata taratibu za kisheria. Shughuli katika mgodi huo hatari zimesitishwa kuzuia maafa zaidi, huku zoezi la uokoaji likiingia siku ya pili.