Manispaa ya Malindi imewakamata watu 2 kwa kosa la kuchafua mazingira baada ya kuunda Mabomba kinyume na sheria na kuelekeza Maji machafu barabarani.
Akithibitisha kisa hicho, maneja wa manispaa ya Malindi Dadu Chome amesema hatua hiyo inafuata msako mkali unaotekelezwa na manispaa hiyo Kwa wafanyibiashara wanaodaiwa kuchafua mazingira eneo hilo.
Kulingana na maafisa hao mabomba yaliyowekwa hayafai kutumiwa kumwaga Maji machafu kwani mbali na kuharibu mazingira, Maji hayo husambaza magonjwa. Wale wanaofanya biashara mbali mbali mjini humo wametakiwa kuweka mikakati ya kudhibiti Maji na taka kutoka Kwa biashara lau sivyo watachukuliwa hatua...