- 6,713 viewsDuration: 3:35Idadi ya waliokufa katika ajali ya barabarani katika eneo la Katumani kwenye barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa imefikia nane. Hii ni baada ya watu wengine wawili kufariki wakitibiwa katika hospitali ya Machakos Level 5. Ajali hiyo ya ijumaa usiku ilihusisha basi la abiria lililokuwa likitoka Mombasa lililogongana na matatu iliyokuwa ikisafirisha abiria kutoka jijini Nairobi kuelekea Pwani