Skip to main content
Skip to main content

Watu saba warekodi taarifa kuhusu kifo cha kijana Park Road

  • | Citizen TV
    11,149 views
    Duration: 3:02
    Watu saba, wakiwemo walinzi wawili wa Katibu wa Wizara ya Michezo na Vijana Fikirini Jacobs, wameandikisha taarifa kuhusiana na kifo cha kijana anayedaiwa kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wa katibu huyo ndani ya gari lake. Cecil Ouma anadaiwa kufariki kufuatia tukio hilo lililotokea katika Barabara ya Park Road jana jioni. Inadaiwa kuwa marehemu aliingia ndani ya gari la Katibu Fikirini na kuzua rabsha baada ya kukamilika kwa mkutano wa vijana katika eneo la Kariokor. Gatete Njoroge anatuarifu zaidi.