Skip to main content
Skip to main content

Watu sita wafariki, wanane wajeruhiwa katika ajali ya matatu tatu Lessos

  • | Citizen TV
    3,403 views
    Duration: 56s
    Watu sita wamefariki huku wengine wanane wakijeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha matatu tatu eneo la Mlima Punda, katika makutano ya Lessos, kwenye Barabara Kuu ya Eldoret kwenda Nakuru usiku wa kuamkia leo. Naibu Kamanda wa Polisi wa Ainabkoi, Charles Getembe, amesema matatu iliyokuwa ikitokea Nakuru kuelekea Eldoret iligonga matatu mbili zilizokuwa zinaelekea Nakuru wakati dereva alijaribu kupita lori. Marehemu walipelekwa katika makafani ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi jijini Eldoret, huku majeruhi wakipelekwa katika Hospitali ya Kaunti ya Burnt Forest.