- 4,656 viewsDuration: 2:37Watu wanne wamekamatwa katika eneo la Bondo, kaunti ya Siaya, kwa tuhuma za kuwachoma watoto wanne kwa maji ya moto. Washukiwa hao, akiwemo kiongozi wa kanisa la St. Abraham Israel Assemblies of God, wanadaiwa kukiri kuwachoma watoto hao kwa kisingizio cha kuwatoa mapepo. Maafisa wa idara ya huduma za watoto kwa ushirikiano na polisi waliwaokoa watoto watatu waliokuwa wamefanyiwa ukatili huo, huku kanisa hilo likifungwa.