- 1,317 viewsDuration: 3:14Watu watano wamefariki katika eneo la Lolgorian, kaunti ya Narok, kufuatia maporomoko kwenye mgodi wa Kilima Pesa. Kufikia jioni ya leo, maafisa wa uokoaji walikuwa wakiendelea kuchimba vifusi vya mgodi huo kuwatafuta watu wengine wanaoaminika kukwama ndani. Hata hivyo, kulikuwa na afueni baada ya mtu mmoja aliyekuwa ndani ya mgodi huo kuokolewa akiwa salama.