- 6,821 viewsDuration: 2:59Watu wawili walifariki na wengine 53 kujeruhiwa wakati wa vurugu zilizokumba mkutano wa Linda Mwananchi katika kaunti ya Homa Bay hapo jana. Kulingana na ripoti kutoka Hospitali ya Rufaa ya Homa Bay, mwanamke mmoja alifariki alipokuwa akitibiwa baada ya kugongwa na gari wakati wa msafara wa Linda Mwananchi mjini Homa Bay. Makumi ya wengine walijeruhiwa, baadhi yao kwa kukatwa kwa mapanga. Haya yanajiri huku manusura wa vurugu hizo wakisimulia yaliyojiri. Laura Otieno anatuarifu.