- 1,437 viewsDuration: 2:48Watu wawili walifariki wakati wa maandamano ya Jumatatu kaunti ya Laikipia baada ya kupigwa risasi na maafisa wa usalama. Familia ya Charles Mwangi inasema kuwa kijana huyo hakuwa akishiriki maandamano dhidi ya ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola katika eneo hilo. Polisi wanadaiwa kufyatua risasi kiholela kuwatawanya waliokuwa wanaandamana. Serikali ya United States imewashauri raia wake kuchukua tahadhari katika maeneo ya Laikipia, Nanyuki na Nairobi kufuatia matukio ya maandamano ya Jumatatu.