Skip to main content
Skip to main content

Wauguzi kaunti ya Embu watishia kuanza mgomo baada ya siku 7

  • | Citizen TV
    236 views
    Duration: 1:57
    Huduma za afya katika Kaunti ya Embu huenda zikatatizika baada ya wauguzi kutoa notisi ya mgomo wa siku saba kwa serikali ya kaunti wakilalamikia kutotekelezwa kwa makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2024. Akizungumza na wanahabari mjini Embu, Katibu wa Muungano wauguzi tawi la Embu, Macharia Kanderi amesema makubaliano hayo yaliitaka serikali ya kaunti kuwapandisha vyeo wauguzi wataalam, wale wenye umri wa miaka 57 na zaidi, na wauguzi ambao wamesalia katika kundi moja la kazi kwa zaidi ya miaka saba licha ya kustahili kupandishwa vyeo pamoja na wauguzi ambao tayari walikuwa wamefikia muda wao wa kupandishwa vyeo. Kanderi amesema kuwa ni moja tu kati ya makubaliano hayo manne ambayo yametekelezwa huku akionya kuwa wauguzi watasitisha huduma iwapo serikali ya kaunti haitachukua hatua katika ndani ya muda wa siku saba.