- 1,070 viewsDuration: 38sWavuvi sita wamesombwa maji katika visa viwili tofauti kwenye fuo za sanda na Mageta, katika ziwa victoria kaunti ya Siaya. Kisa cha kwanza kilitokea kwenye ufuo wa Sanda, ambapo wavuvi watano walisombwa maji baada ya boti walimokuwa ndani kuanguka ziwa victoria. Miili ya wavuvi wawili imefikishwa kwenye makafani ya Got Agulu, huku shughuli ya kutafuta miili ya wavuvi watatu ikiendelea.